1. UTANGULIZI
Mkataba huu unajulikana kama Mkataba wa Hali Bora unaohusisha masuala ya ajira na mahusiano kazini kati ya mwajiri yaani Said Salim Bakhresa & Co Ltd (SSB & CO. LTD) na tawi la chama cha Wafanyakazi wa Viwanda, Biashara, Taasisi za Fedha, Huduma na Ushauri (TUICO) yaani wawakilishi wa wafanyakazi.
Kwamba sisi SSB &Co Ltd tujulikanao kama mwajiri kwa upande mmoja na Tawi la chama cha wafanyakazi wa viwanda, biashara, taasisi za fedha, huduma na ushauri ( TUICO) Tawi la chama cha wafanyakazi kwa upande mwingine tunakubaliana mambo yafuatayo:
- Kwamba kwa hiyari yetu wenyewe tumekubaliana mambo yafuatayo;-
- Kwamba mwajiri anatambua kuwa TUICO ndicho chombo ambacho kinawakilisha wafanyakazi katika masuala ya utetezi na maslahi ya wafanyakazi kwenye Kampuni yake.
- Kwamba TUICO inatambua kuwa SSB & Co Ltd (Mzizima) ndiye mwajiri aliyewaajiri wafanyakazi wanachama wa TUICO na ana mamlaka kuhusu ajira na maslahi ya wafanyakazi.
2. KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA
Pande zote mbili zimekubaliana kwamba kima cha chini cha mshahara ni Tsh 150,000/=(Laki moja na elfu hamsini tu) kuanzia tarehe 01. 03. 2012.
3. LIKIZO
Pande zote mbili tumekubaliana kuwa
Kila mwaka mfanyakazi atakuwa na haki ya kwenda likizo na atakuwa na haki ya kupata Tsh 120, 000/=(Laki moja na ishirini) wakati atakapo kuwa anakwenda likizo yake ya mwaka (Annual leave), malipo ambayo yatajulikana kama posho ya likizo (leave allowance). Utaratibu huu pia utaanza kutumika 01. 03. 2012.
4. KIFO
Pande zote mbili tumekubaliana kwamba:
i. Endapo mfanyakazi atafariki mwajiri atatoa Tsh 500, 000/- ambazo ubani na gharama za mazishi.
ii. Endapo mfanyakazi atafiwa na mke, mume, mtoto wa kumzaa mwenyewe, baba mzazi, au mama mzazi,
mfanyakazi huyo atapewa rambirambi ya Tsh 200, 000/=(Laki mbili tu)
5. MFANYAKAZI HODARI
Pande zote mbili tumekubaliana kwamba:-
i. Inapofika wakati wa sherehe ya sikuu ya Mei Mosi kila mwaka mwajiri atakuwa na haki ya kutoa mfanyakazi hodari ambaye atakuwa anachaguiiwa kwa kushirikiana na Tuico na Mwajiri.
ii. Mfanyakazi bora wa kampuni atazawadiwa na mwajiri Tsh 500, 000/=(Laki tano)
iii. Mfanyakazi bora wa idara atazawadiwa na mwajiri Tsh 200, 000/=(Laki mbili)
6. MUDA WA MKATABA
Pande zote mbili tumekubaliana kuwa muda wa mkataba ni miaka miwili (2) kuanzia tarehe 1/3/2012 mpaka tarehe 1/3/2014
7. MASURUFU (ALLOWANCES)
i. Kodi ya nyumba Tsh 40, 000/= kila mwezi
ii. Nauli Tsh 30, 000/= kila mwezi
8. MENGINEYO
Pande zote mbili tumekubaliana kwamba:-
i. TUICO watazingatia kanuni na sheria zote za kazi za hapa nchini.
ii. Wafanyakazi watazingatia kuwa lazima wafikie lengo la ubora wa bidhaa na kuzalisha kwa kiwango cha juu cha mashine (Quality products and full capacity of machine)
9. HITIMISHO
Mkataba huu umethibitishwa na kusainiwa leo tarehe .../.../ 2012
Kwa upande wa TUICO:
Kwa upande wa Mwajiri:
Umesainiwa kwa niaba ya SAID SALIM BAKHRESA & CO. LTD:
Jina
Jina…………………………………………………..
Sahihi
Cheo