MKATABA WA UTAMBUZI NA HALI BORA ZA KAZI (COLLECTIVE BARGAINING AGREEMENT) BAINA YA CHAMA CHA MAWASILIANO NA UCHUKUZI TANZANIA [COTWU (T)] NA KAMPUNI YA SMB NYEHUNGE EXPRESS

New1

1.0 UTANGULIZI

1.1 Sisi Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania, tujulikanao hapa kama "Chama cha Wafanyakazi" na Kampuni ya SMB Nyehunge Express tujulikanao hapa kama "Mwajiri" kwa hiari zetu na katika hali ya maelewano, tumefikia makubaliano katika masuala yaliyomo kwenye kumbukumbu hii, ambayo yanaweka utambuzi na hali bora zaidi za kazi, kwa wafanyakazi walioajiriwa na Kampuni hii.

2.0 UTAMBUZI

2.1 Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania [COTWU (T)], kinaitambua Kampuni ya SMB Nyehunge Express kuwa amewaajiri wafanyakazi ambao pia ni wanachama wake; Kadhalika Kampuni wanaitambua COTWU (T), kuwa ndicho chombo pekee cha wafanyakazi kinachotetea haki na maslahi yao.

2.2 Kwa ujumla kila chombo kimoja kinatambua kuwepo kwa chombo kingine kisheria na kwamba wafanyakazi hawa ni kiungo kikubwa cha ushirikiano baina yao.

3.0 WAHUSIKA

3.1 Mkataba huu utawahusu wafanyakazi wote wa Kampuni ya SMB Nyehunge Express isipokuwa wale wenye mkataba maalum ambao si raia wa nchi hii (Expertriate); maana ya wafanyakazi kwa mujibu wa mkataba huu ni Wafanyakazi wote.

4.0 KUANZA NA KUDUMU KWA MKATABA

4.1 Pande zote mbili katika Mkataba huu, tunakubaliana kwamba Mkataba huu uanze kutumika tarehe 01/09/2011 na kudumu kwa miezi ishirini na minne (24).

4.2 Upande wowote utakaokusudia kufuta, kuongeza, kupunguza au kurekebisha kifungu chochote katika mkataba huu unaweza kufanya hivyo kwa kuupa kwanza taarifa ya mwezi mmoja, upande wa pili na kuelezea sababu za makusudi hayo.

4.3 Mkataba huu utaendelea kuheshimiwa hata baada ya muda uliowekwa katika kifungu 4.1 cha ibara hii, iwapo hapatakuwepo na upande utakao toa taarifa kwa upande mwingine kwa makusudi ya kutengeneza upya Mkataba huu.

5.0 AJIRA NA MAJARIBIO

5.1 Wafanyakazi wa kudumu wa Kampuni hii wataajiriwa kwa mshahara wa mwezi katika masharti ya kudumu baada ya kupitia utaratibu wa majaribio katika ajira zao.

5.1.1 Majaribio: - Wafanyakazi wote watakuwa katika kipindi cha majaribio ya miezi sita (6) kabla ya kuthibitishwa katika ajira zao.

5.1.2 Kuthibitishwa:- Baada ya kumaliza vyema muda wa majaribio Mfanyakazi atapata barua ya kuthibitishwa katika ajira.

5.1.3 Mfanyakazi ataachishwa kazi katika kipindi cha majaribio iwapo hatafanya vizuri katika majaribio yake.

5.2 Kutothibitishwa kwa mfanyakazi kwa makosa ya mwajiri hakutachukuliwa kuwa mfanyakazi hajamaliza majaribio vizuri.

5.3 Ajira ya vibarua (kutwa) itaendelea kuwepo tu kwa zile kazi zisizodumu kwa zaidi ya miezi mitatu (3) na za dharura.

6.0 KUACHA AU KUACHISHWA KAZI

6.1 Kama kutakuwepo sababu ya kumwachisha kazi mfanyakazi, taarifa ya kuachishwa itatolewa kwa utaratibu unaoelekezwa na ibara hii.

6.1.1 Mfanyakazi akiacha/kuachishwa kazi taarifa ya mwezi mmoja itatolewa au mshahara badala yake.

6.1.2 Mfanyakazi anayeachishwa kazi baada ya kumaliza miaka mitano (5) katika utumishi atalipwa mshahara wa mwezi mmoja mara miaka ya utumishi wake kazini (SMB Nyehunge Express).

7.0 UPUNGUZAJI WA WAFANYAKAZI

7.1 Pande zote zinakubaliana kulinda nafasi za kazi zilizopo na kufanya kila juhudi kuzuia uwezekano wa kupunguza wafanyakazi ambao wana nafasi zao tayari katika ajira.

7.2 Upunguzaji wa wafanyakazi utachukuwa nafasi tu, baada ya uongozi wa Kampuni kushauriana na viongozi wa Tawi la COTWU (T) na Kanda COTWU (T), na baada ya kufikiria njia mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo ikiwa ni pamoja na kuwahamisha wafanyakazi kutoka idara moja kwenda nyingine, mpaka hapo itakapokuwa hali nzuri au kama lazima kwa kuwapunguza kidogo kidogo.

7.3 Ikiwa njia zote zitashindikana kwa kadri ya ujio wake, Kampuni itafuata utaratibu wa FILO (first in last out) katika kupunguza wafanyakazi.

7. 4 Pamoja na zoezi hilo masuala muhimu yafuatayo yatatakiwa yatazamwe kwanza:-

7.3.1 Juhudi katika kazi

7.3.2 Uzoefu na Uhodari

7.3.3 Uwezo wa kufanya kazi

7.3.4 Uaminifu na Nidhamu.

7.5 Wale wote watakaopunguzwa kazi wawe wa kwanza kurejeshwa kazini hali ya Kampuni inapokuwa nzuri, kwa kuzingatia vifungu vidogo 7.3.1 - 7.3.4 (ibara ya 7.4).

7.6 Kampuni itawajibika kuwalipia nauli zao, familia na mizigo kwa viwango vifuatavyo:-

7.5.1 Wafanyakazi wa kawaida watasafirishiwa mizigo kwa kiasi cha tani mbili (2) kwa kila atakayepunguzwa kazi

7.7 Mfanyakazi ambaye atapunguzwa na mwajiri, asipolipwa malipo yake kwa wakati huo huo, basi baada ya juma moja lenye siku saba (7) tangu kupunguzwa kazi, mwajiri atalazimika kumlipa mfanyakazi huyo posho ya kila siku sawa na mshahara wake wa kutwa mara tatu (kutwa x moja).

7.8 Mfanyakazi atakayepunguzwa kazi atalipwa mshahara wake wa miezi miwili mara miaka ya utumishi ili mradi utumishi wake sio chini ya mwaka mmoja.

8.0 SAA ZA KAZI NA MALIPO YA ZIADA

8.1 Saa za kazi za kawaida zitakuwa arobaini na tano (45) kwa juma moja lenye siku za kazi sita (6); Siku za Jumapili na Sikukuu zinazotambulika na Taifa, zitakuwa ni siku za mapumziko.

8.2 Saa zote za ziada zinazozidi arobaini na tano (45) za muda wa kawaida wa kazi ’zitachukuliwa kuwa za malipo ya ziada (overtime); Kazi itakayofanyika nyakati za siku za kazi na sikukuu zitakuwa na malipo kwa utaratibu ufuatao:-

8.2.1 Kwa siku za kawaida za kazi malipo ya ziada yatakuwa maaium kwa kulipwa mara moja na nusu (1/130) ya mshahara kwa saa wa mfanyakazi.

8.2.2 Kazi itakayofanyika katika siku za mapumziko na sikukuu, mfanyakazi atalipwa malipo maaium kwa kulipwa mara mbili (2) (1/90) ya mshahara kwa saa wa mfanyakazi.

8.2.3 Pande zote tumekubaliana kwamba malipo hayo katika 8.2.1na 8.2.2 yatatolewa kila siku/yatakuwa ya kila mwezi.

9.0 VIMA VYA MISHAHARA NA NYONGEZA KWA WAFANYAKAZI

9.1 Mishahara italipwa kwa wafanyakazi ambao wataajiriwa, kwa mujibu wa makubaliano yetu; Kima cha chini cha mshahara wa kampuni kitakuwa shilingi laki moja na nusu (150,000/=) kwa mwezi. Mishahara mingine itapangwa kwa ushirikiano wa mwajiri, uongozi wa Tawi la COTWU (T) na Kanda kwa madhumuni ya kutofautisha kazi za ujuzi na taaluma mbalimbali za wafanyakazi wa Gereji na Mabasi.

9.2 Pande zote katika Mkataba huu tumekubaliana kuwa nyongeza za mishahara zitatolewa mwezi Januari kila mwaka. Lakini mwajiri anaweza kuongeza mshahara kwa mfanyakazi mmoja au kikundi (section) kabla ya kufika mwaka mzima tangu kutolewa nyongeza zilizopita ikiwa mfanyakazi au "section" inayohusika watakuwa wamefanya kazi ya kuvutia/kujitokeza kwa faida na manufaa ya kampuni ya SMB Nyehunge Express.

9.3 Kwa maana ya ibara 9.2 ya mkataba huu, Kampuni kwa kushirikiana na Tawi la COTWU (T), watakutana kutayarisha viwango vya nyongeza kwa asilimia sio chini ya kumi na tano (15%) itakayo kubaliwa na pande hizo mbili kutegemea pato la mwaka husika kisha kutoa taarifa kwa Katibu Mkuu na Kanda, miezi mi-wili kabla ya nyongeza kwa ajili ya majadiliano.

10.0 KUSTAAFU

10.1 Pande zote mbili tunakubaliana kwamba, kila mfanyakazi atakuwa na umri wa kustaafu ambao utafikia, au anaweza kustaafu mapema endapo afya yake kwa kuthibitishwa na daktari itaonekana haimwezeshi kuendelea na kazi yoyote.

10.2 Mfanyakazi hataendelea kufanya kazi baada ya umri wa miaka sitini (60), umri kati ya miaka hamsini na mitano (55) na hamsini na tisa (59), mfanyakazi anaruhusiwa kustaafu kwa hiari na kulipwa haki zake zote.

10.3 Kwa makubaliano na mwajiri wake, mfanyakazi anaweza kuendelea na Utumishi wa Mkataba Maalum baada ya kustaafu kwa lazima na kulipwa haki zake zote.

10.4 Mfanyakazi anayestaafu kwa umri wa lazima atalipwa mshahara wa miezi nne (4) mara (x) miaka ya utumishi wake kuwa shukrani kwa utumishi mzuri na uvumilivu wake kazini. Pamoja na malipo mengine mwajiri atamlipa mfanyakazi anayestaafu gharama zote za usafiri wake, familia na mizigo yake hadi Kijijini kwake.

11.0 POSHO KWA KAMATI YA TAWI LA COTWU (T)

11.1 Kwa kuwa viongozi wa Chama cha Wafanyakazi daima hufanya shughuli za manufaa kwa Kampuni na wafanyakazi kwa muda wote hata baada ya saa za kazi; Pande zote tumekubaliana kuwa viongozi hao wapatiwe malipo kidogo kama posho ya kila mwezi kwa kutambua umuhimu wa shughuli zao.

11.2 Kamati ya Tawi la COTWU (T) watalipwa posho ya shilingi elfu ishirini (20,000/=) kila mwezi kwa kuzingatia makubaliano haya.

12.0 LIKIZO YA MWAKA NA GHARAMA ZAKE

12.1 Katika kipindi cha miezi kumi na miwili (12) ya utumishi mfululizo, mfanyakazi atakuwa na haki ya kupumzika kwa siku thelathini (30) Malimbikizo ya likizo yatakubaliwa ikiwa mfanyakazi ataomba kwa maandishi na kukubaliwa na uongozi, au iwapo uongozi utamtaka abakie kazini kwa sababu ya shughuli nyingi za kikazi.

12.2 Likizo ya mwaka itakuwa ni ya malipo kamili; Mbali na kulipwa ujira sawa na siku zake za mapumziko; mfanyakazi atalipwa nauli yake yeye na familia yake kwenda likizo na kurudi kazini kila mwaka.

13.0 POSHO YA SAFARI ZA KIKAZI.

13.1 Pande zote tumekubaliana kuwa mfanyakazi anapokwenda safari ya kikazi nje ya kituo cha kazi atalipwa posho ya safari.

13.2 Mfanyakazi Dreva/Fundi akisafiri kikazi atastahili kulipwa posho ya shilingi elfu kumi (10,000/=) sawa na gharama za nyumba ya wageni (Guest House) kila siku.

13.3 Pande zote tumekubaliana kuwa iwapo mfanyakazi atakuwa katika safari hiyo ya kikazi kwa zaidi ya mwezi mmoja, atalipwa mara mbili ya mshahara wake wa kawaida wa mwezi, ili kumwezesha kukidhi mahitaji ya nyumbani kwake na kujikimu nje ya kituo cha kazi.

13.4 Wafanyakazi ambao hawakutajwa humu watalipwa kwa kutumia ibara 13.2.1 ya Mkataba huu.

14.0 MICHANGO YA WANACHAMA.

14.1 Michango ya mwanachama wa COTWU (T), itakatwa kutokana na asilimia mbili (2%) au itakayoamuliwa na vikao vya juu vya Chama kutoka katika mapato ya mshahara wa kila mwanachama, na kiasi hicho kama huduma za Chama cha COTWU (T) (service fees) kwa mfanyakazi asiye mwanachama wa COTWU (T); Na kuwasilishwa kwenye Makao Makuu ya COTWU (T), kwa kupitia A/C Na. 019103005914 iliyoko Benki ya Taifa ya Biashara Tawi la Kichwele, S. L. P. 9044, Dar es Salaam, kabla ya tarehe saba (7) ya mwezi unaofuatia ule wa makato.

14.2 Inatambulika na kukubalika kwamba kutokuwasilisha michango hiyo kwa wakati unaotajwa 14.1, Mwajiri atapaswa kulipa pamoja na adhabu ya asilimia saba (7%) ya michango ya mwezi iliyocheleweshwa kuwasilishwa.

15.0 GHARAMA ZA MAZISHI

15.1 Gharama za mazishi zitatolewa kwa mfanyakazi anayefariki akiwa bado katika utumishi, au jamaa ya mfanyakazi mke/mume au mtoto.

15.2 Mwajiri atatoa pamoja na gharama zingine zote, usafiri wa mwili wa marehemu hadi anakotakiwa kuzikwa na ndugu zake.

15.3 Pande zote tumekubaliana kuwa mwajiri atasafirisha vyombo vya marehemu hadi kwao pamoja na kutoa kiasi cha shilingi laki moja (100,000/=) kuwa rambirambi.

16.0 TIJA NA UFANISI

16.1 Pande zote katika Mkataba huu tunakubaliana kuwa Tija na Ufanisi vitapimwa na kufanyiwa mikakati, ili kuhakikisha kuwa uhai wa Kampuni unakuwepo kufuatia Tija ya kutosha.

16.2 Kwa kuzingatia ibara hiyo 16.1 hapo juu, uongozi wa Kampuni wataandaa malengo ya kazi kwa kila mwaka, (miezi miwili) kabla ya kipindi cha mwaka wa fedha cha Kampuni kuanza na kuwaalifu COTWU (T) Tawi na Kanda.

16.3 Pande zote zitashirikiana kwa karibu katika kuhakikisha kwamba malengo yaliyowekwa yanakamilishwa na hata kuvukwa.

16.4 Pande zote tumekubaliana kuwa kila miezi mitatu kitafanyika kikao cha pamoja cha pande hizi mbili za Mkataba huu ambacho kitahusisha Menejimenti ya Kampuni, COTWU (T) - Kanda na Tawi ili kutathimini Tija na Mapato na ili kuziwezesha pande hizi kupanga viwango vya Bonus; Kwa maana hiyo kila mwaka itatolewa Bonus kwa kadri ya faida kwa kampuni.

17.0 PANGO LA NYUMBA

17.1 Pande zote tumekubaliana kwamba kila mfanyakazi atalipwa kiasi cha asilimia kumi (10%) ya mshahara wake kila mwezi, kuwa pango la nyumba ili mradi mfanyakazi huyo haishi kwenye nyumba ya mwajiri ama kupangishiwa na mwajiri.

18.0 SAREZAKAZI

18.1 Pande zote za Mkataba huu tumekubaliana kwamba, wafanyakazi walio katika taaluma zifuatazo watastahili kupatiwa SARE za kufanyia kazi kila mwaka pea mbili.

18.1.1 Walinzi - Overoll pamoja na koti la mvua

18.1.2 Madreva - Kaunda suti

18.1.3 Mafundi - Overol -Gum boots

18.2 Ili kuziweka nadhifu nguo za kazi kila mfanyakazi atapatiwa sabuni

miche miwili kwa kila mwezi.

19.0 SARE NA ZAWADI ZA MEI MOSI

19.1 Utakapofika wakati wa sherehe za Mei Mosi ya kila mwaka, uongozi wa Kampuni kwa kushirikiana na Tawi la COTWU (T), wakizingatia maelekezo ya Katibu wa Kanda - COTWU (T). Watakaa kuteua mfanyakazi BORA mmoja na mfanyakazi HODARI mmoja ambao watazawadiwa siku ya kilele cha sherehe hizo (tarehe 1/5).

19.2 Kwa maana ya uteuzi huo, mfanyakazi BORA atazawadiwa laki mbili na kuendelea, mfanyakazi HODARI wa Kampuni atazawadiwa shilingi laki mbili (200,000/=).

19.3 Pande zote tumekubaliana kuwa kiongozi wa Tawi la COTWU (T) na mwakilishi wa uongozi wa Kampuni ambao watawasilisha zawadi za wafanyakazi watakazo zawadiwa mbele ya mgeni rasmi siku ya kilele cha Mei Mosi, watashonewa Kaunda Suti kwa ajili ya sherehe hiyo na kwa heshima ya Kampuni yao.

20.0 MWENENDO WA MASHAURI NA MIGOGORO

20.1 Mashauri na migogoro yoyote ya kikazi itakayotokea mahali pa kazi kati ya mwajiri na mfanyakazi au wafanyakazi wenyewe; Sheria mpya ya Kazi na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004, na ama kama zitakavyofanyiwa marekebisho na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zitatumika kwa kadri ya ujio wa mashauri/migogoro hiyo.

20.2 Pande zote tumekubaliana kwamba mgogoro wa kikazi au mfarakano utashughulikiwa na Tawi la COTWU (T), mahali pa kazi kwanza. Hakuna upande wowote utakaofikia Matumizi ya Sheria zilizotajwa na ibara hii (para 1) kabla ya kushindikana kwa usuluhishi ambao utafanywa na ofisi ya COTWU (T) Kanda.

20.3 Mgogoro wa kikazi utapatiwa ufumbuzi wake wa kisheria, ama mbele ya msuluhishi (CMA) au inapolazimika na Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi.

20.4 Tumekubaliana kuwa Uamuzi wa Mahakama kwa mujibu wa Mkataba huu utaheshimiwa kuwa ni wa mwisho bila kuomba Rufaa mahali popote.

21.0 LIKIZO YA UGONJWA NA MALIPO

21.1 Pande zote za Mkataba huu tunakubaliana kwamba, mfanyakazi atapatiwa likizo ya ugonjwa na malipo endapo atapatwa na maradhi akiwa katika utumishi wa Kampuni; Kwa uzingatifu wa ibara hii pande zote mbili tunakubaliana kwamba mfanyakazi atastahili likizo ya ugonjwa na malipo kwa utaratibu na viwango vifuatavyo:-

21.1.1 Mfanyakazi atapata mapumziko pamoja na malipo kamili ya mshahara kwa miezi mitatu (3).

21.1.2 Endapo mfanyakazi hatapona kurejea kazini, atapatiwa mapumziko mengine na nusu (1/2) ya mshahara kwa miezi mingine miwili (2).

21.1.3 Baada ya kipindi hicho ikiwa mfanyakazi hatapona, mwajiri anaweza kumwachisha kazi na kumlipa stahili zake zote kwa mujibu wa Mkataba huu.

21.1.4 Likizo hiyo ya ugonjwa haitahusishwa wala kuathiri likizo nyingine za mfanyakazi.

22.0 LIKIZO YA UZAZI.

22.1 Pande zote mbili za Mkataba huu, tumekubaliana kuwathamini na kuwapa heshima na utambuzi uwapasao wanawake katika ajira zao, kwa makusudi ya kuiaani unyanyasaji wa kijinsia.

22.2 Kwa kuzingatia ibara hii 28.1 hapo juu, pande zote tumekubaliana kuwa likizo ya uzazi itakuwa ni ya siku mia moja (100) kuanzia tarehe ya kujifungua kwa mfanyakazi, na malipo ya likizo yatatolewa mara moja.

22.3 Kwa kutambua kuwa kwa mujibu wa sheria, likizo hii ya uzazi hutolewa mara moja kila baada ya miaka mitatu. Pande zote mbili tumekubaliana kuwa mfanyakazi atakayepata ujauzito kila baada ya miaka mitano ya utumishi tangu kuchukua likizo kama hiyo, Kampuni itamlipa mshahara mmoja (1) kama kichocheo cha kuimarisha Kampeni ya Taifa ya Uzazi wa Mpango na kujenga vyema afya ya mama mzazi na mtoto.

22.4 Mfanyakazi ambaye ataweza kuhudhuria kazini kwa siku zote za uja uzito hadi juma la mwisho la kujifungua, atapatiwa posho ya likizo hiyo sawa na mshahara wake wa mwezi mzima.

22.5 Likizo ya uzazi inaweza kuanza mwezi mmoja kabla ya kujifungua kwa mtumishi ikiwa Daktari ataamua hivyo.

23.0 MIKOPO YA SIKUKUU

23.1 Pande zote tumekubaliana kuwa mwajiri atawapatia wafanyakazi wake huduma inayowapa heshima inayofaa. Hivyo kwa mujibu wa makubalianao haya mwajiri atawapa wafanyakazi mikopo ya kuwawezesha kukidhi mahitaji ya sikukuu zote za kidini.

23.2 Katika kila sikukuu moja ya hizo hapo juu (za kidini) kila mfanyakazi anayetaka atakopeshwa mshahara wake wa miezi miwili (2) kuwa mkopo wa sikukuu.

23.3 Pande zote tumekubaliana kuwa mkopo wa sikukuu utarejeshwa katika kipindi cha miezi minne (4).

23.4 Pamoja na uzingatifu wa ibara hii hapo juu (23.3) mfanyakazi hatazuiwa kuagiza akatwe mshahara kwa ajili ya kurejesha mkopo kwa kipindi kilicho chini ya muda wa makubaliano haya.

24.0 CHAKULA CHA MCHANA

24.1 Pande zote katika Mkataba huu tumekubaliana kwamba Mwajiri atatoa chakula cha mchana, kwa wafanyakazi wanaoendelea na kipindi cha mchana kwa wale wafanyakazi wa Gereji na Ofisini.

24.2 Kwa maana ya mkataba huu mwajiri atatoa gharama sawa na shilingi elfu moja na mia tano (1,500/=). Kila siku kwa mfanyakazi anayetajwa kifungu 24.1.

25.1 Pande zote katika Mkataba huu tumekubaliana kwamba Kwa ajili ya kuthibitisha makubaliano ya pande hizi mbili za Chama na Mwajiri hapa chini tunatia saini zetu mnamo leo hii tarehe 15 mwezi 08 mwaka 2011 mahali Nyehunge - Mwanza

Kwa niaba na kwa ajili ya chama

1.Sahihi

]ina: SAID MOHAI

Cheo: MKURUGENZI

Jina: JONATHAN MAZULA MAKONGORO

Cheo: KAIMU KATIBU WA KANDA Cheo: MENEJA UTAWAULA

Jina: ATHUMANI ISSA SELEMANI

Cheo: MWENYEKITI WA TAWI

Jina: ZOLLO BUYAh Cheo: KATIBU WA TAWI

TZA Kampuni Ya SMB Nyehunge Express - 2011

Start date: → 2011-09-01
End date: → 2013-08-31
Ratified by: → Ministry
Ratified on: → 2011-08-15
Name industry: → Transport, logistics, communication
Public/private sector: → In the private sector
Concluded by:
Name company: →  Kampuni Ya SMB Nyehunge Express
Names trade unions: →  COTWUT - Muungano wa Wafanyakazi wa Usafiri na Mawasiliano wa Tanzania

SICKNESS AND DISABILITY

Maximum for sickness pay (for 6 months): → 50 %
Maximum days for paid sickness leave: → 150 days
Provisions regarding return to work after long-term illness, e.g. cancer treatment: → 
Paid menstruation leave: → No
Pay in case of disability due to work accident: → No

HEALTH AND SAFETY AND MEDICAL ASSISTANCE

Medical assistance agreed: → No
Medical assistance for relatives agreed: → No
Contribution to health insurance agreed: → No
Health insurance for relatives agreed: → No
Health and safety policy agreed: → No
Health and safety training agreed: → No
Protective clothing provided: → 
Regular or yearly medical checkup or visits provided by the employer: → No
Monitoring of musculoskeletal solicitation of workstations, professional risks and/or relationship between work and health: → 
Funeral assistance: → Yes

WORK AND FAMILY ARRANGEMENTS

Maternity paid leave: → 14 weeks
Maternity paid leave restricted to 100 % of basic wage
Job security after maternity leave: → Yes
Prohibition of discrimination related to maternity: → No
Prohibition to oblige pregnant or breastfeeding workers to perform dangerous or unhealthy work: → 
Workplace risk assessment on the safety and health of pregnant or nursing women: → 
Availability of alternatives to dangerous or unhealthy work for pregnant or breastfeeding workers: → 
Time off for prenatal medical examinations: → 
Prohibition of screening for pregnancy before regularising non-standard workers: → 
Prohibition of screening for pregnancy before promotion: → 
Facilities for nursing mothers: → No
Employer-provided childcare facilities: → No
Employer-subsidized childcare facilities: → No
Monetary tuition/subsidy for children's education: → No

EMPLOYMENT CONTRACTS

Trial period duration: → 180 days
Part-time workers excluded from any provision: → 
Provisions about temporary workers: → 
Apprentices excluded from any provision: → 
Minijobs/student jobs excluded from any provision: → 

WORKING HOURS, SCHEDULES AND HOLIDAYS

Working hours per week: → 45.0
Working days per week: → 6.0
Paid annual leave: → 30.0 days
Paid annual leave: → 5.0 weeks
Paid bank holidays: → Good Friday, Easter Monday, Human Rights Day / Vernal Equinox Day / Iraq's Spring Day / Namibia Independence Day (21st March), Army Day / Feast of the Sacred Heart/ St. Peter & Paul’s Day (30th June), Chile Independence Day (18th September), Pentecost Monday / Whit Monday / Monday of the Holy Spirit (day after Pentecost / seventh Monday after Easter)
Rest period of at least one day per week agreed: → Yes
Maximum number of Sundays / bank holidays that can be worked in a year: → 
Provisions on flexible work arrangements: → 

WAGES

Wages determined by means of pay scales: → No
Provision that minimum wages set by the government have to be respected: → 
Adjustment for rising costs of living: → 0

Wage increase

Wage increase: → 15.0 %

Extra payment for annual leave

Extra payment for annual leave: → TZS 10000.0

Premium for overtime work

Premium for overtime work: → 150 % of basic wage

Premium for Sunday work

Premium for Sunday work: → 200 %

Meal vouchers

Meal allowances provided: → Yes
→ 1500.0 per meal
Free legal assistance: → 
Loading...