Kima cha Chini cha Mishahara nchini Tanzania - Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

Je kuna sheria tofauti inayohusiana na kima cha chini Tanzania?

Sheria ya Taasisi za Kazi, Nambari 7 ya mwaka wa 2007 kati ya mambo mengine hutoa Kima cha Chini. Kijumla, sheria hii inachofanya ni kwamba huweka Taasisi zote za Sheria, kutoa kwa utendaji wao, nguvu na wajibu na masuala mengine yanayohusiana nao. Bodi ya Mapato ni moja ya Taasisi, na inaunda sehemu ya V ya sheria. Chini ya sehemu hii vitengo vya Bodi kadhaa za Mapato huteuliwa na Waziri na zinawezeshwa kuchunguza ajira na sheria na masharti ya ajira katika vitengo tofauti na kuripoti matokeo na mapendekezo kwa waziri. Kutoka kwa matokeo Waziri anawezeshwa na Sheria sawa baada ya kuangalia mapendekezo kutoa Agizo la Mapato kuamua kima cha chini na hali zingine za ajira ya wafanyakazi katika kitengo chochote cha uchumi. Kisha agizo linalojulikana kama agizo la Usimamizi wa Mapato na masharti ya ya ajira (Agizo la Mapato) linawekwa na kuchapishwa kupitia Noitisi ya Serikali. Agizo sasa linaweka kitengo cha Kima cha chini. Kima cha chini cha kitengo hutolewa chini ya Sehemu A ya Agizo la Usimamizi wa Mapato na masharti ya Ajira (Agizo la Mapato). Kwa sasa hii inafanywa kwa agizo la GN 196 ambalo lilichapishwa mnamo Juni 28, 2013.

Je kuna kima cha chini kima au zaidi ambacho kinaamuliwa na sheria?

Kima hiki cha chini huwepo kulingana na vitengo tofauti na vikuu vya uchumi. Hata hivyo sio vitengo vyote hushughulikiwa. Kwa sasa tuna idadi ya vitengo 8 na baadhi ya vitengo viliyo na ugawanyaji/uainishaji na kima 15 tofauti cha chini hutolewa chini ya sheria hiyo ni, agizo la Kusimamia Mapato na masharti ya ajira, 2010.

Ni katika kiwango kipi kima cha chini huamuliwa?

Kima cha chini huamuliwa kwa kitengo hiyo ni kulingana na kitengo cha uchumi wa biashara. Kwa kuwa tuna na vitengo 12 Waziri anateua bodi 12 za mapato kila moja imewezeshwa kuchunguza ajira na masharti mengine ya ajira na kutuma mapendekezo kwa Waziri. Agizo la sasa la Kima cha Chini lina vitengo kumi na mbili ambavyo ni: Huduma za Afya, Huduma za Kilimo, Biashara, Huduma za Kiwanda na Biashara, huduma za Mawasiliano, Huduma za Uchimbaji madini, shule za Kibinafsi, Huduma za Nyumbani na Hospitali, Huduma za Usalama wa Kibinafsi, huduma za Nishati, Huduma za uchukuzi, Huduma za Utegaji samaki na Bahari na huduma za Ujenzi. Baadhi ya vitengo vina uainishaji mdogo kama invyoonekana katika jedwali ya kima cha chini.

Je kima cha chini huhesabiwa katika msingi upi?

Kima cha chini huhesabiwa kila saa, kila siku, kila wiki, kila wiki mbili na kila mwezi. Imeundwa katika njia ambayo inaangalia uwiano kati ya gharama ya maisha na uwezo wa biashara kulipa na kudumisha. Kwa hivyo sio mchakato rahisi ili usifanye iwe vigumu kwa waajiri au wafanyakazi.

Katika hali ya kima cha chini cha kila wiki/kila mwezi, je hulingana na idadi ya saa ya kudumu?

Ndio, Kima cha Chini huhesabiowa kwa saa 45 kwa kila wiki. Kulingana na kitengo cha 19 cha Sheria ya Ajira na Uhusiano wa Kazi, 2004 saa za kawaida za kazi ni saa 45 kwa wiki na saa tisa katika siku. Na siku sita katika wiki.

Je mashirika ya serikali, mwajiri na/au washirika wa chama cha wafanyakazi wanahusika katika mpango wa kima cha chini?

NDIO, mwakilishi wa waajira, chama cha wafanyakazi na serikali wanahusika katika uwekaji wa kima cha chini. Kitengo cha 35 (3) cha Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004 inatoa uwekaji wa bodi ya mapato kwamba itakuwa na Mwenyekiti (kawaida ni serikali) na mwanachama aliyeteuliwa na shirika la Waajiri Kitaifa na shirika la Kitaifa la Chama cha Wafanyakazi kila moja kuwakilisha hisia za waajiri na wafanyakazi.

Je ustawishaji (Marekebisho) wa kima cha chini huamuliwa aje?

Marekebisho hufanywa na Waziri baada ya kupata mapendekezo kutoka kwa Bodi tofauti za Mapato kama ilivyotolewa chini ya Agizo la Usimamizi Mapato na masharti ya ajira, 2013.

Ni vipi vijenzi vya Kima cha Chini Tanzania?

Kulingana na Agizo la Usimamizi Mapato na masharti ya ajira, Gn 196, 2013 vitengo vya vijenzi/mapato vya bodi ya Agizo la Mapato zinajumuisha Huduma za Afya, Huduma za Kilimo, huduma za Mawasiliano, Huduma za Nyumbani na Hospitali, Usalama wa Kibinafsi, huduma za Nishati, Huduma za uchukuzi, huduma za Ujenzi, Uchimbaji madini, Shule za Kibinafsi, Huduma za Biashara, Kiwanda na Biashara; Utegaji samaki na Bahari.

Je kijenzi cha kudumu cha kima cha chini hupandishwa daraja mara ngapi?

Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004 haitoi muda wa kupandisha daraja kima cha chini. Hata hivyo Bodi za Mapato vinawajibu wa kuchunguza chochote kuhusu ajira na masharti ya ajira ikiwa ni pamoja na kupandisha daraja vijenzi vya Agizo la Kima cha Chini. Mwaka huu (2013), kima cha chini kimesahihishwa na agizo mpya la nambari GN 196.

Ni kipimo kipi ambacho ustawishaji kima cha chimo hufanywa?

Sehemu ya 37 ya Sheria ya Taasisi ya Kazi, inatoa ya kwamba katika uchunguzaji wowote wa kima cha chini kilichopendekezwa, Bodi ya Mapato itaangalia sababu muhimu kama vile, uwezo wa mwajiri kufanya biashara yao kwa mafanikio, utendakazi wa biashara ndogo, wastani na kifogo, gharama ya maisha, kuzidi kwa umasikini, kiwango cha chini cha kijingujiko, ajira na sheria na masharti ya ajira ya wafanyakazi walioajiriwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, maafikiano yeyote yanayotoa ajira na sheria na masharti ya ajira katika kitengo, kifungu 22 na kifungu 23 cha Katiba ya Muungano wa Jamuhuri ya Tanzania (hii inatoa Haki ya Kufanya kazi na kumiliki mali), Mapatano yeyote au mapendekezo ya ILO na sababu yeyote muhimu.

Kiwango cha Umasikini Kitaifa ni upi?

Bonyeza hapa kujua laini ya Umaskini wa Taifa katika mazingira na kiwango cha chini cha Mshahara, Mishahara Hai na Mishahara Halisi. Changua fedha (Euro au fedha ya taifa) upate kujua laini ya Umaskini wa Taifa.

Tokeo la kima cha chini katika uajiri wa kitaifa (wanaopokea mapato tu) ni lipi?

Haitumiki

Ufikiano wa Kima cha Chini hudhibitiwa aje?

Ridhaa ya Kima cha Chini inasimamiwa kupitia Idara ya Usimamizi Kazi na Huduma za Ukaguzi ambayo iko chini ya Wizara ya Kazi na Ajira. Idara inasimamiwa na Kamishna wa Kazi. Maafisa wa Kazi chini ya idara hii wamewezeshwa na Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004 ili kusimamia ridhaa na viwango vya ajira ikiwa ni pamoja na Agizo la Kima cha Chini na sheria na masharti mengine ya ajira.

Ni vikwazo vipi vya kisheria vinaweza kutumika ikiwa hakuna ufikiano?

Kwanza kabisa ikiwa Afisa wa Kazi anaamini ya kwamba mwajiri hajafuata sheria za kazi anaweza kutoa agizo la ridhaa na ikiwa mwajiri anashindwa kufuata agizo la kisheria mwajiri atashtakiwa na akifungwa atalipa faini isiyozidi Shilingi Millioni Tano, kifungo cha kipindi cha miezi 3 au zote faini na kifungo. Hii ni kulingana na kitengo 64 (2) cha Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004.

Je vikwazo hutumika mara kwa mara?

Tuna kesi chache ambapo vikwazo vimetumika kwa kuwa kesi chache zinashtakiwa.

Je wawakilishi wa mwajiri na au chama cha wafanyakazi huhusika katika utaratibu wa kuafikiana?

sio hivyo, uhusika uko katika kiwango cha ukaguzi, wakiwa katika maeneo ya kazi Wachunguzi wa Kazi uhoji wafanyakazi au chama cha wafanyakazi ikiwa wako na mwakilishi wa usimamizi. Hata hivyo ikiwa kuna mzozo wa haki au wafanyakazi waliosajiliwa chini ya chama cha wafanyakazi wanaweza kwenda kwa Tume kwa Upatanisho na Usuluhishi kupitia tawi lao. Waajiri pia wanaweza kwenda kwa Tume kwa Upatanisho na Usuluhishi kupitia mashirika ya waajiri wao.

Ni kwa nani/wapi watu binafsi wanaweza kulalamika, ikiwa wanafikiria wanapokea mapato ya chini kuliko kima cha chini?

Watu binafsi wanaweza kulalamika au kuripoti mzozo ili kudai baki kwa Tume la Upatanisho na Usuluhishi (CMA) wenyewe au kupitia vyama vyao vya wafanyakazi. CMA ni taasisi ya kazi iliyoanzishwa chini ya sehemu ya 12 ya Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004 na kazi ya kupatanisha mzozo wowote uliotajwa katika masharti ya sheria yeyote ya kazi; kuamua mzozo wowote uliotajwa na Usuluhishi. Kamshina wa Kazi 12 chini ya sehemu 47 (8) ya sheria ya taasisi ya kazi, 2000 inatumika kwa Mahakama ya Kazi kulazimisha ufuataji ikiwa mwajiri hajafuata agizo. Na ridhaa yake inaweza kuripotiwa katika mahakama ya Kazi pia kulingana na Sheria ya Taasisi ya Kazi, 2004.

Loading...